Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Duru za hospitali nchini humo zimesema idadi ya vifo huenda itaongezeka kutokana hali mbaya ya majeruhi wa ajali hiyo ya juzi Jumamosi.
Mripuko huo ulipelekea nyumba na viwanda vilivyokuwa karibu kuanguka na kufunikwa na wingu jeusi la moshi mbali na kuharibu magari kadhaa.
Baada ya kushika mto, lori hilo lilipoteza mwelekeo na kuingia katika duka lililokuwa karibu na kusababisha mripuko. Video iliyosambazwa na shirika la habari la CGTN la China inaonyesha moto mkubwa ukiwaka huku watu wakipiga kamsa na mayowe.
Ajali za namna hii zimekuwa zikiripotiwa mara kwa mara nchini China. Machi mwaka jana, watu karibu 80 walipoteza maisha katika mripuko mwingine uliotokea katika kiwanda cha kemikali cha Jiangsu Tianjiayi huko Yancheng katika kaunti ya Xiangshui mashariki mwa China.
Mripuko mkubwa zaidi ulioshuhudiwa nchini China katika miaka ya hivi karibuni ni ule wa mwaka 2015 katika eneo la Tianjin, ambao uliua watu 173.
342/